Muigizaji wa filamu za bongo Yusuph Mlela amefunguka na kumtaka Nay wa Mitego kuheshimu kazi za watu wengine na kama yeye ameshafanikiwa kimaisha basi awapishe watu wengine waendelee kujitafutia riziki.
Akizungumza kwenye eNewz ya EATV Mlela amesema kwamba Nay anapaswa kuacha kufuatilia mambo yasiyo muhusu na aendelee na shughuli zake za uimbaji au akae pembeni.
'Mimi namuomba sana Nay ajiheshimu sana, asiingilie kazi za watu ambazo hazimuhusu. kama yeye ameshajiweza kwenye suala la kipato basi akae pembeni atuache wengine tutafute riziki"- alisema Mlela.
Aidha Mlela ameongeza kuwa "Sawa mimi na yeye tunaweza tukawa hatulingani labda kiuwezo na kimaisha kwa sababu yeye anaona tayari amekwisha rizika, ndio maana namuomba tupande ulingoni ili tuheshimiane. Mimi kama ningekuwa naimba ningeingia studio nikatengeneza wimbo wa kumchana lakini kwa vile kazi zetu haziingiliani ndiyo maana nasisitiza ki Hip hop tuu tuingie ulingoni ili heshima iwepo tuache maneno maneno"- Mlela aliongeza.
Aidha Mlela amekanusha kauli ya kuitwa mtoto wa kike na Nay na kumgeuzia kibao kwa kudai mtu anayeisifu mvua sana huenda ikawa imemnyea ndio maana kutwa anaizungumza kauli ya kumfananisha na mwanamke.
0 comments:
Post a Comment