
Mwigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu.
DAR ES SALAAM: Baada ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuvaa
nguo zenye rangi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) alipotinga mahakamani
hivi karibuni angali ni mwanachama damu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kisha baadhi ya wafuasi kudai anawasaliti, uongozi
wa chama hicho umemtolea tamko.
ILIKOANZIA
Wema
hivi karibuni akiwa ameongozana na mama yake, Miriam Sepetu na mashosti
zake wengine, alitinga kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar kwenye ile kesi yake ya ‘unga’ akiwa amevaa gauni refu la njano, juu
akiwa amevaa ‘koti laini’ lenye rangi ya kijani na wekundu kwa mbali,
hali iliyoibua mjadala kwa wafuasi wa Chadema waliokuwa mahakamani hapo.
“Huyu
mbona leo katuvalia nguo hizi? Hizi si rangi za CCM kabisa? Mh! Kwa
hili siyo sawa kabisa,” alisikika akisema mwanamke mmoja aliyekuwa
amevaa magwanda ya Chadema.
Mwingine
akadakia: “Ni kweli rangi siyo ishu lakini kwa yeye ambaye juzijuzi
alitangaza kuwa sasa ni Chadema damu, mavazi ya rangi hizi angeyachukia,
sasa ona, utadhani ni kada wa CCM bwana.”
Kutokana
na suala hilo kuibua maswali mengi kwa baadhi ya wanachama wa Chadema
waliokuwa mahakamani hapo, Risasi Jumamosi liliwatafuta baadhi ya
viongozi wa Chadema na kuwauliza kuhusiana na suala hilo ambapo kila
mmoja alitoa tamko lake.
Meya
wa Ubungo ambaye ndiye mlezi mkuu wa Wema Sepetu, Boniphace Jacob
alisema; “Chadema siyo nguo, ni imani na itikadi kwani mahakamani lazima
avae sare za Chadema? Hizo ni nguo tu kamanda, siyo ‘big deal’ sana.”
Kwa upande wa msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alieleza; “Hivi
wale mashabiki au wanachama wa Simba wakivaa nguo za njano au kijani kwa
sababu yoyote ile huwa ni ‘puppets’ (vibaraka) wa Yanga? Nadhani majibu
hayo yamejitosheleza.”


0 comments:
Post a Comment