Thursday, May 4, 2017

Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini ameuawa kwa kupigwa risasi mjini
Mogadishu. Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais. Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia. Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.

Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri.
Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma.
 

Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.
Huyo ni waziri wa Somalia

0 comments:

Post a Comment