
IGP mpya wa jeshi la polisi amewaita waandishi na kwanza ameomba ushirikiano wa waandishi wa habari uendelee kama walivyompa aliepita. Amesema anawahakikishia swala la Ikwiriri na Rufiji ni la muda mfupi na yeye na timu yake ndani ya Jeshi la polisi ni lazima watapata majibu, amesema kikundi cha watu wachache hakiwezi kuwafanyia watanzania ubaya.
Amesema wanapeleka salam kuwa ubaya wanaoufanya waujibu kwa ubaya kwa mujibu wa sheria. Kuhusu wanaotumia bodaboda kufanya uhalifu, amesema hakuna mtu alie juu ya sheria. Amesema bodaboda wanapita kwenye taa nyekundu, wanapita wakiwa kwenye mshikaki. Amewapa salam kuwa ni wakati wa utii wa sheria. Amesema watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya waache. Watu wenye hasira kali nao wameguswa akitolea mfano wezi wa kuku na kuhoji kama kuku ana thamani sawa na mhusika.
Amesisitiza kama amekosa akamatwe na apelekwe mahakamani na kusema anayejifanya ana hasira kali itamfanya aiache familia yake. Kuhusu askari kujihusisha na rushwa, amesema hakuna askari atakaejihusisha na Rushwa na akabaki salama na kusema ameshatoa maelekezo kwa jeshi polisi kuwa atakaefanikisha kupatikana kwa wala rushwa atapata zawadi. Ameahidi milioni kumi kwa atakaetoa taarifa sahihi kwa watu wa Kibiti, mwisho amewatakia mfungo mwema walio kwenye swaum.
0 comments:
Post a Comment