Thursday, May 11, 2017

Ikiwa tunaelekea katika msimu mpya wa Coke Studio Africa mwaka 2017, siku chache zilizopita tuliwashuhudia watanzania Rayvanny wa WCB Wasafi pamoja na Aika na Nahreal ambao wanaunda kundi la Nay Kenzo wakikinukisha katika studio za Coke Studio jijini Nairobi nchini Kenya.

Time hii ni Mtanzania mwingine kutoka A List ya wana bongo fleva, Izzo Bizness ambaye wiki iliyopita kupitia ukurasa wake wa instagram ndio alitusanua kwa good news mwaka huu naye amepata shavu la kukinukisha kwenye Coke Studio.
Tayari Izzo amekwisha kuwasili pande hizo na kuanza kukinukisha kama kawiz, na mapicha picha tumekwisha anza kuyaona kupitia kurasa zake za kijamii.

0 comments:

Post a Comment