*10/05/2017 Mkoa wa Pwani.*
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka
Hamdu Shaka (MNEC) Leo amendelea na ziara katika Halmashauri ya Wilaya
ya Chalinze, kukagua utekelezaji wa ilani, uhai wa CCM na jumuiya zake
na kupata taarifa ya maendeleo ya uchaguzi.
Pia lipata nafasi ya
kuzungumza na makundi ya vijana, viongozi ngazi ya shina hadi Wilaya wa
chama na jumuiya zake, kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika
miradi ya maendeleo ya ujenzi wa tangi la maji shule ya sekondari Moreto
uliogharimu jumla ya T.sh 50 millioni, ujenzi wa kituo cha Polisi cha
Lunga ambacho hadi hatua iliyofikia kinajengwa kwa nguvu za wananchi na
wahisani .
Aidha alikabidhi
kwa madiwani wa kata 15 wa jimbo la Chalinze cement pkt 2,287 zenye
thamani ya 22,013,500/ Mabati 633 yenye thamani ya T.sh 14,559,000/
fedha taslim 5,650,000/ na fedha kwa ajili ya usafiri 3,800,000/
vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe Ridhwani J. Kikwete
ukiwa ni ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi iliyoanzishwa
katika kata hizo.
*"Katika jambo kubwa la kihistori alilofanya
Mhe Rais Magufuli ni kuteuwa RC, MADC, DED na DAS vijana, maeneo mengi
niliyokwisha tembelea mambo yako vizuri sana, vijana wenzetu
mnatuwakilisha na mnamuwakilisha Mhe Rais vilivyo tunajivunia utendaji
wenu, Wilaya ya Bagamoyo na halmashauri zake zote mbili mumejipanga na
mnakimbizana na kasi ya kupeleka maendeleo endelevu kwa wananchi
kijamii na kiuchumi.*
*nimesikiliza taarifa ya mkuu wa wilaya na
watendaji wa halmashauri kwa umakini na nimebahatika kutembelea baadhi
ya miradi iliyoanzishwa na serikali na ile ya nguvu za wananchi ninyi
hamna maneno mengi vitendo vya kazi ndio vingi.*
*endeleeni
kulinda heshima hii ninakupongeza sana Alhaj Majid na wakurugenzi wako
wote wawili, wasaidizi wenu na waheshimiwa madiwani mumejiongeza na
mmekuwa wabunifu hii ndio faida ya kuwa na madiwani wote toka CCM
wanaojitambua*
*nilikotembea katika maeneo mengine sijasikia
wenyeviti wa vijiji wakilipwa posho kama sehemu ya kuwafanya kuongeza
kazi ya kuwatumikia wananchi na kuwafanya wache kuingia katika migogoro
isiyo na lazima kwa tamaa, ni kweli mkijipanga vizuri katika kusimamia
mapato yenu hakuna lisilowezekana.*
*nimejionea mipango mizuri
mnayoendele kuitekeleza ambayo inaonesha wazi kuwa mumedhamiria
kikweli kufanya mageuzi ya kimfumo katika kuharakisha upatikanaji wa
maendeleo kwa wananchi.*
*haya ndio mambo ya kuwaeleza wananchi
ambayo yamefanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya awamu ya tano
inayongozwa na Dk John Pombe Magufuli."* Sehemu ya hotuba ya Kaimu
Katibu Mkuu wakati alizungumza na viongozi wa mashina, tawi, kata,
wenyeviti wa vijiji, maafisa watendaji wa vitongoji, vijiji na kata
pamoja na madiwani wa kata 35 za jimbo la Chalinze na viti maalum
wanawake".
Kaimu Katibu Mkuu amemaliza ziara katika Wilaya ya Bagamoyo na kesho ataendelea Wilaya ya Kibaha Vijijini.
|
0 comments:
Post a Comment