Leo katika Mahakama ya Kisutu, inaendelea kesi ya Jamhuri dhidi ya
Wakurugenzi wa Jamii Media, ambayo ni kesi namba 458 ya Mwaka 2016.
![[IMG]](https://i0.wp.com/zanzibar24.co.tz/wp-content/uploads/2017/02/mello2.png?resize=462%2C588)
Katika kesi hii, Wanashtakiwa kwa makosa mawili:
1) Kuendesha mtandao ambayo haujasajiliwa nchini do-tz, yaani .tz (Tanzania domain).
2) Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.
Habibu Rashid Ntahigie ndo shahidi wa kwanza leo. Huyu ni Meneja wa Rejistry ya .tz. Elimu yake ni masters ya IT na management, Ila professionally ni mhandisi wa umeme. Yuko hapo tangu 2008 kampuni ilipoanzishwa na ni mwajiriwa wa 1 wa kampuni.
Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti. tzNIC inasimamia rasilimali mojawapo ya mawasiliano tanzania yani kikoa cha .tz....rasilimali nyingine ni +255. Watanzania wamepewa herufi 2 wazitumie wakati wanatumia mitandao.
Wakili wa Serikali anayeitwa Salum anauliza: Wadau wenu wakubwa ni nani? Au taasisi gani zinatumia hiyo .tz?
Kwa mujibu wa EPOCA imeainishwa kuwa taasisi zote za serikali na binafsi zinasisitizwa/kuhimizwa kutumia .tz
Salum: Dhumuni ni nini?
Shahidi: 1. Identity kwenye mtandao
2. Credibility kwenye mtandao
Lengo lingine kubwa ni kupunguza gharama za mawasiliano kwenye mtandao.
Salum: Usajili umeanza rasmi lini?
Shahidi: 2009....
Salum: Ukiangalia upande wa pili wa mahakama (upande wa watuhumiwa) kuna unayemfahamu?
Shahidi: Ndio namfahamu Maxence Melo
Salum: Ulimuona wapi?
Shahidi: Kwenye press conference ya kutangaza kikoa cha .tz New Africa Hotel mwaka 2010.
Salum: Ulifahamu anahusika na nini?
Shahidi: Wakati ule sikujua...ila baadae nilijua kuwa ana mtandao anaendesha.
Nafahamu kuwa anaendesha mtandao wa Jamiiforums.com
Salum: Wamewahi kujisajili kwenu?
Shahidi: Ndio wamesajili majina mawili, JF.co.tz na jamiiforums.co.tz
Salum: Unakumbuka walisajili lini?
Shahidi anataka arefresh memory sababu hakumbuki accurately.... (anataka kusoma)
Wakili wa JamiiForums anasema lazima na yeye aone atakachosoma..
Lissu anasema: Hicho atakachosoma ni lazima iwe alikiandika muda huo tukio lilipotokea...hivyo lazma waone asije kuwa kaandaliwa notes
Wakili wa serikali amewithdraw ombi la shahidi la kurefresh
Shahidi: sikumbuki Vizuri Tarehe lakini ilikuwa 2013...zikisajiliwa miezi tofauti...2016 zikafutwa miezi tofauti, Baada ya kama mwezi mmoja zilisajiliwa tena 2016. Sasa hivi ziko kwenye database, moja inaexpire June mwaka huu nyingine November.....
Salum: Kwahiyo sasa hivi ziko mbili kwenye database?
Kibatala: that was a leading Question.
(Wamevutana kidogo)
Salum: Tuhuma zilizopo mahakamani umezisikia?
Shahidi: Nimesikia kuwa mtuhumiwa hatumii kikoa cha .co.tz
Salum: Ulichukua hatua gani baada ya kusikia hvyo??
Shahidi: Nilienda kuhakikisha kama wamesajili?? Nikakuta ndio wamesajili. Ila katika kuhakiki kama wanatumia nimegundua jf.co tz wala jamiiforums.co.tz hazitumiki.
Nimeangalia kama yanatumika kwa barua pepe lakini hayana MS request...hivyo hayatumiki. Hivyo wamesajili lakini hawatumii kwa barua pepe wala tovuti. Kitaalamu hiyo inaitwa 'domain parking' yani kuzuia mtu asitumie jina lako
Salum: Zaidi ya kikoa cha .tz kuna vikoa vingine vinavyotumika kwenye mtandao?
Shahidi: Vipo vingi kama .com ambayo ni generic top level domain .com inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za marekani, .tz inaendeshwa kwa mujibu wa sheria za tanzania.
Wakili wa serikali ameuliza swali ila kaambiwa abadilishe aina ya maswali kwani ilikuwa leading question
Salum: Baada ya kuanzishwa kwa sheria, je vipi kuhusu vikoa vingine?
Shahidi: Sheria haijaongelea vikoa vingine bali imesisitiza tu matumizi ya .tz.
Advocate Peter Kibatala kaingia kufanya cross examination ya shahidi
Kibatala: Shahidi umesema wewe ni meneja wa tznic??
Ndio
Kibatala: Je tukitaka kuhakikisha wewe ni meneja utatusaidiaje?
Inabidi umuulize mwajiri wangu
Kibatala: Kwahiyo hapo uliposimama hatuwezi kujua?
Sijabeba kitambulisho (kaweka mikono mfukoni hakimu kamwambia aitoe)
Kibatala: Kampuni yenu ni registry, je mna register/registers?? Yaani mna sehemu ambapo tukitaka kujua huyu kajisajili huyu hajajisajili tunaweza kwenda??
Ndio papo...
Kibatala: Je mahali hapo panaitwaje??
Kibatala: Ukienda kwenye tovuti yetu tznic.org.tz ukurasa wa 1 kabisa ukiweka jina litakupa jibu.
Kibatala: Je ni nani custodian wa mahali huko??
Kila kikoa kina custodian wake...Pia kama ni mtaalam ukienda kwenye platform ya unix unaweza kuingiza domain name kwenye who is.com
Kibatala: Kutokana na maelezo yako nimeelewa kuwa hakuna issue ya non-compliance kwa kusajili upande wa jamiiforums, ni kweli?
Ni kweli
Kibatala anaonesha document....."shahidi naomba utuambie kama hii ndio extract ya who is unayozungumzia"
Ni kweli hii ni extract ya who is...
Kibatala: inaonesha nini hapo kuhusu jamiiforums??
Inaonesha jina jamiiforums.co.tz limesajiliwa june 2016..
Kibatala: Je hiyo jamiiforums.co.tz kama inavyoonekana hapo imekidhi vigezo vya kisheria vya kiusajili??
Nilishatoa ufafanuzi hapo awali kuwa wamesajili majina mawili...lakini sheria inaongelea kuhusu usajili na utumizi
Kibatala: Je uko tayari kuikabidhi hii document kwa hakimu(extract ya whois) ili itumike kama kithibitisho cha yale uliyosema??
Shahidi: sina kipingamizi...ni public info
Wakili wa serikali: shahidi yuko kizimbani lakini anatuwakilisha sisi...hii document iko mtandaoni na hatujui imetolewaje huko....hata muhuri ni wa jamii media..hawana authority ya kucertify hii document.
Kibatala: sijaona objection ya kisheria..shahidi ambae ni mtaalamu wa IT ameitambua na hajaikosoa na ameomba ipokelewe kama ilivyo...Shahidi ni shahidi wa anayoyafahamu na ndio maana ameapishwa yeye...kazi ya upande uliomuita ni kumprompt kueleza anayoyafahamu...So hakuna uwakilishi wa shahidi...na hii inaondoa hata objection iliyowekwa... Mradi shahidi ameiown hiyo document naomba ipokelewe km exhibit PI...
Upande wa Serikali: hii document ni copy...original document iko kwenye whois...hii copy lazima iwe certified.
Hakimu kasema kwakuwa kuna vifungu wametaja itabidi akavipitie kwani sheria ya ushahidi kwa mambo ya mtandao imechange hivyo atavipitia ili ajue km ataipokea hyo document au la.
Hakimu: Tarehe 5 mwezi wa 6 tutatoa uamuzi na shauri litaendelea...shahidi naomba ufike siku hiyo....

0 comments:
Post a Comment