
Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.
Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya
shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema jana
Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari
wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya
ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko kwenye
hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa kulipa
Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo
na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu
kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa
kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata
rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo
Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa
za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo mtu asiwe
mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje
ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema.
Awali akifungua
semina hiyo, Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo
kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika
kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa
huduma stahiki kwa wananchi.
“Najua
kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi
watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu
walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia
taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi,Alisema Bw. Kayombo.
Bwana Kayombo
amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya
kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na
taasisi za umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema
na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya
kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka
kwa watalamu wa kodi wa TRA.
0 comments:
Post a Comment