Baada ya picha kuzagaa katika mitandao mbalimbali zikimuonesha Scott Disick akifurahia mahusiano yake mapya huko Cannes Villa nchini Ufaransa hatimaye makubwa yaibuka.
Mrembo huyo mwenye miaka 19, raia wa Kidachi ameibuka na kumshutumu mpenzi wake huyo ambaye alikuwa akitoka na Kourtney Kardashian kuwa anamtumia tu ila hana mapenzi naye. Bella amesema kuwa Scott amemdanganya na alikuwa na kimwana mwingine ambaye yupo naye Cannes.
Picha zilizozagaa zilimuonesha Scott akiwa na mwanamke mwingine maeneo ya Canne Villa ila sio Bella Throne “Scott alinifuata Los Angles (LA) na nikaaminisha yupo serious kuwa na mahusiano na mimi na nikamuamini,sikuwa na wazo la kuwa na mahusiano” amesema Bella alipokuwa akiongea na mtandao wa TMZ.
Hatimaye muigizaji huyo wa tamthilia ya ‘My Own Worst Enemy’ ametambua kuwa Scott amemtumia kujifariji na machungu ya kuachwa kutokea familia ya Kardashian.
0 comments:
Post a Comment