Baada ya Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee kupewa adhabu ya kutoudhuria vikao vyote vya bajeti katika bunge linaloendelea sasa Dodoma kufuatia Mbunge huyo kubainika alitukana bungeni, Bunge limemsamehe Mbunge huyo na kumpa masharti.
Wabunge wengi walisimama bungeni na kumuombea msamaha Halima Mdee kwa kitendo chake hicho kwa kuwa mbunge huyo alikwisha omba radhi mbele ya bunge hilo na kwa wananchi.
Kufuatia zoezi hilo la wabunge kumuombea radhi Bunge liliazimia kuwa kiongozi huyo asamehewe na kupewa masharti kuwa endapo akifanya kosa lolote lingine Bungeni atachukuliwa hatua na spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kufuatia maamuzi haya Mbunge Halima Mdee ambaye ni Waziri Kivuli wa Fedha ataendelea kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment