Saturday, May 13, 2017

Mtayarishaji wa muziki wa Singeli kutoka De Fetality Studio, Mesen Selekta amedai muziki wa sengeli ni muziki ambao haumkatai mtu huku akidai hata mgumu kama Nikki Mbishi akiamua kuingia kwenye muziki huo anaweza kufanya vizuri.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Mesen amedai muziki wa Singeli ni muziki wa kawaida ambao anaweza kuufanya msanii yoyote huku akidai utofauti unazalishwa kwenye beat.
“Huu muziki hata Nikki Mbishi akitaka kuufanya anaweza akaufanya vizuri mpaka watu wakashanga,” alisema Mesen. “Muziki ni ule ule utofauti unakuja kwenye beat, kama beat ya hip hop inapiga mara mbili kwa wakati mmoja, beat ya Singeli itapiga mara nne kwa sababu ni muziki ambao unaenda haraka zaidi,”
Aliongeza, “Ndio maana nawashangaa sana watu wanaomsema vibaya Professor Jay, Professor ni yule yule alichobadilisha kwenye ule wimbo ni beat tu lakini Professor Jay kachana kama kawaida na watu wameona. Kwa hiyo mimi naweza kusema kwamba wasanii wote tunatakiwa kuupa support muziki wa Singeli ili ufike mbali zaidi, anapotokea mtu anaonesha nia ya kusaidia na kukuza muziki wa Singeli halafu mtu anaponda sio vitu vizuri,”
Pia mtayarishaji huyo amedai muziki wa Singeli umeweza kupiga hatua kwa kiasi fulani ndani ya muda mfupi huku akidai kuna baadhi ya wasanii wa muziki huo wanalipwa mpaka milioni 4 kwa show.

0 comments:

Post a Comment