Posted by Williammalecela.com on Thursday, May 25, 2017
*RC Gambo akutana na Kamisha Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji*
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo amekutana na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ndg. Thobias Andengenye ofisini
kwake. Katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana
katika kufanya kazi na pia jeshi la zimamoto na uokoaji wameomba
ushirikiano toka kwa mkuu wa mkoa ili kuweza kuliunganisha jeshi hilo na
mamlaka za serikali za mitaa ili liweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwani mnufaika mkubwa wa huduma zao ni mamlaka hizo husika.
Mhe. Mrisho Gambo ametoa rai kwa Jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa
mazoea badala ya kusubiri matukio ya ajali za moto kutokea wanapaswa
kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuyazuia matukio hayo na kwa kufanya
hivyo watapunguza sana kazi yao kwani majanga ya moto yatakua historia.
Pia wamekubaliana kuhakikisha ramani za majengo na michoro ya mpango
kabambe (master plan) kwa jiji la Arusha zinapitiwa, lengo ni kuona
mapungufu ya kiusalama dhidi ya majanga ya moto na kuona namna ya
kuzitatua mapema. Mkoa wa Arusha hasa kwa jiji la Arusha ni miongoni
mwa maeneo ambayo kuna changamoto kubwa sana hasa panapotokea majanga
ya moto kwani miundo mbinu na vituo vya zimamoto havitoshelezi mahitaji.
0 comments:
Post a Comment