Friday, May 5, 2017

Rapa chipukizi kutoka Mwanza asiyekaukiwa na malalamiko, Edu Boy amewachana wasanii wa Bongo kuwa ni wanafiki na hawana ushirikiano kwani wamekuwa wakilalamika kwenye kundi la simu 'Whatsapp group' huku wakitoka hadharani wanajikausha.

Akizungumza na eNEWZ ya EATV, Eddu Boy, ameweka wazi kuwa wasanii wengine wamekuwa wakimpongeza kwenye simu kwa kuwachana baadhi ya wasanii wasiotoa sapoti kwa wenzao kupitia wimbo wake wa Naiee na hata mtandaoni.
"Ni wanafki kwa sababu wanasema nalalamika lakini baadae anakuja ananisifia Edu boy noma lile goma lako umelinyoosha linaenda safi sana lakini wakiingia huku wanalalamika, mfano Shilole alikuja akasema kwenye group jamani kama msiponiungisha, kula siyo tatizo hata kupost joint yangu mnashindwa halafu mnasema umoja ni nguvu? Huyu huyu Shilole ndiye aliniambia Edu By kupostiwa siyo lazima, mimi nasema hivi wasanii ni wanafki"- alifunguka Edu Boy.
Akizungumzia suala la kumlalamikia Vanessa Mdee, Eddu Boy, ameweka wazi kuwa, Vanessa Mdee, alimpa jibu baya na ndio maana ameamua kulalamika zaidi kuhusiana na yeye kumpotezea.
"Vanessa ni dada yangu napofanya kazi ni mtu ambaye ninahitaji msaada wake kwakuwa amefanya ngoma na watu kama AKA akiwa kama dada yangu sio lazima apost ila akipost itasaidia sana... Niliona ngoja nimkumbushe a-post cover ya wimbo wangu akanijibu kuwa nisimsumbue na ki cover changu". Amesema Eddu Boy.
Eddu Boy anatajwa sana kama mmoja wa wasanii anayeongoza kwa kulalamika ila yeye ameamua kuweka wazi kuwa anaongea ukweli ambao upo na siyo kutafuta kiki.

0 comments:

Post a Comment