Msanii wa muziki, Msami amefunguka kwa kudai kuwa ubinafsi na kukosa ushirikiano miongoni mwa wasanii ni moja kati ya sababu zinazowafanya ya wasanii wa muziki kushindwa kufanya vizuri kimataifa.
Msami amedai muziki kutopiga hatua zaidi kimataifa kumetokana na baadhi ya wasanii wanaofanya vizuri kimataifa kuwa wabinafsi kwa kushindwa kutoa nafasi kwa wengine.
“Kukosa ile roho ya kuwa na umoja na ukweli ndani ya nafsi yako. Tunafanya vitu vinakwama unaaza kujiuliza mwenyewe umekwama kwa sababu gani unagundua ninakosa ushirikiano, unarudi mwenyewe unanza kutengeneza ushirikiano na watu. Hata kama unataka kwenda kimataifa na huku ndani huna ushirikiano hata mashabiki nao watajigawa ndio unakuta wanapambana mtu fulani akose tuzo nje,” amesema Msami alipokuwa akizungumza na Times Fm.
0 comments:
Post a Comment