Thursday, May 4, 2017

Msanii machachari wa muziki, Vanessa Mdee, amedai anaongelewa maneno machafu na mmoja kati ya vigogo anaowaheshimu kwenye sanaa ya muziki nchini, hali iliyomsukuma kuanika ya moyoni.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Duasi’ alioshirikishwa na Legendary Beatz, ametumia mtandao wa Twitter kuyatoa ya moyoni dhidi ya mwanamuziki huyo, ingawa hakuweka wazi jina lake.
“Inasikitisha kwamba mtu ninayemheshimu na kumtambua kwenye hii sanaa kila kukicha jina langu mdomoni mwake kwa kashfa zisizoeleweka,” alitweet Vanessa.
Hata hivyo, muimbaji huyo ameamua kuweka heshima yake mbele na kujiepusha na majibishano kwani kufanya hivyo anaamini ni utovu wa nidhamu.
“Siwezi kujibishana na wewe itakuwa utovu wa nidhamu baba.,” alitweet tena muimbaji huyo.
Muimbaji huyo anaendelea kukubalika ndani na nje ya nchi ambapo amekuwa akipewa mashavu kadhaa kung’arisha nyimbo za wasanii wa nchi za Afrika Kusini na Afrika Magharibi.

0 comments:

Post a Comment