Posted by Williammalecela.com on Monday, May 08, 2017
 |
UPINZANI NA SIASA NYEPESI
Na Thade Ole Mushi
Wamekosa cha kuzungumza, wamekosa cha kuwaambia wananchi, ahadi zao hazijakamilika, wameamua kufanya siasa Nyepesi.
Eti kwa nn Makamu wa Raisi aje kuaga miili badala ya Raisi.
Hii kwa sasa ndio kick yao, ndio sera yao, ndio mazungumzo yao nk.
Acheni kutumia Msiba wa Arusha kisiasa. Mama Samia ana hadhi inayokaribiana kabisa na raisi kasomeni katiba ya nchi.
Cheo cha Uraisi ni Taasisi Raisi ameshafuata taratibu zote za kutoa
pole, Raisi kashaonyesha ni kiwango gani ameguswa na msiba huu. Taasisi
ya Uraisi inaona mama Samia anatosha kuiwakilisha Ofisi ya Raisi.
Kwenye Tetemeko Kagera Ofisi ya Rais ilimtuma waziri mkuu na alitosha
kabisa kwa shughuli ile. Watu wapo kwenye majonzi nyie mnaleta siasa
...... katiba yetu inatambua hadhi ya makamu wa Raisi.
SEHEMU YA PILI MAKAMU WA RAIS
Ibara ya 47.
Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais
kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan- (a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano; (b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais; (c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
Kwa sera zenu hizi Ikulu mtaikuta kuzimu....
Ole Mushi.
|
0 comments:
Post a Comment