Tuesday, May 30, 2017

Image result for mwanasheria mkuu wa serikali images

 
Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG), George Masaju, alisema ni mapema mno kuanza kuitupia lawama serikali kuhusu hatua hiyo, kwani endapo kutatokea tatizo lolote lazima litafanyiwa kazi.


 

Alisema suala hilo ni nyeti na linagusa maslahi ya nchi, hivyo linapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote. “Hoja kwamba nchi itashtakiwa haina mashiko kwani utekelezaji wa maagizo ya Rais yalizingatia sheria na mikataba iliyopo ambayo imetoa mwanya wa kufanyiwa 'review' kila baada ya miaka mitano,” alieleza.

Aliwataka wabunge hao kuacha kuchangia kwa kuwaogopesha wananchi kwamba nchi iko katika hali mbaya, jambo ambalo si kweli kwani taratibu zote zilifuatwa na nchi iko tayari kushughulikia changamoto zozote zitakazojitokeza.

“Serikali imefanya vyema katika hili kwani hata wenzetu tumewaambia tulichokiona na sasa tunasubiri tuwaambie nini kifanyike kuweka mambo sawa,” alisema. Kuhusu hali ya uwekezaji, alisema si kweli kuwa mazingira ya uwekezaji yameharibiwa na hatua hiyo ya Rais, kwani kwa sasa hali ni nzuri na wawekezaji wameendelea kuja nchini kila kukicha.

0 comments:

Post a Comment