![]() |
Leo
asubuhi nilifuatilia matibabu ya Mzee Francis Maige Ngosha (aliyebuni
Nembo ya Taifa). Anasema alishirikiana na Ndg. Ali Panga Mazanga kwenye
kazi hiyo.
Mwenzake ni marehemu kwa sasa. Hali yake ni dhoofu sana na anahitaji huduma ya Karibu ya wataalamu. Nimemhamishia Muhimbili National Hospital ambako anafanyiwa uchunguzi wa kina. Baada ya kupata ufumbuzi wa tatizo la #afya yake, tutakuwa tumejipanga juu ya namna ya kumhudumia. Itoshe kusema kuwa, Mzee huyu, kama ilivyo kwa wazee wengine, ana haki ya kupata huduma zote za kibinadamu zenye staha sawa na wanadamu wengine. Serikali inaahidi kumhudumia. #HK #Dr_Kigwangalla #HamisiKigwangalla #MzeeWaField #SiasaNiVitendo |
![]() |



0 comments:
Post a Comment