Sunday, May 14, 2017

Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva P Funk Majani amefunguka na kutoa heshima kwa rapa Darassa kutokana na ngoma yake ya 'Muziki' ambayo imeweza kumfanya P Funk kupata mizuka na kudondosha beat 'Wape' kazi ya kundi lililopo chini yake.

P Funk Majani anasema alikata tamaa juu ya muziki wa bongo fleva na kudai wasanii wachache ambao wameweza kuipigania bongo fleva na kufungua milango nje ya Tanzania ndiyo wamemuamasisha zaidi kurudi katika muziki na kuanza upya huku akiwa na ndoto ya kuiteka Afrika kiujumla. 
"Nimependa sana wasanii wengine waliofungua milango na kujulikana nje ya Tanzania hivyo mimi naona fursa kutokana na kipaji changu na uwezo wangu wa kutengeneza wasanii, naweza kujitahidi kutanua wigo, kwanza natakiwa kushika nchi yangu kwanza tena, halafu nianze kufungua milango Kenya, Rwanda, Burundi halafu naanza kuhamia Afrika ya Kusini, Nigeria mwisho wa siku Afrika sababu nataka kuitawala Afrika hiyo ndiyo ndoto yangu na mbele ya Mungu naamini inawezekana" alisema P Funk 
Mbali na hilo P Funk anasema ujio wa kazi hii ya kwanza kutoka kwa wasanii wake wanaounda kundi la 'Bongolos' imechangiwa zaidi na Darassa 
"Nampa respect nyingi sana Darassa yeye ni namna moja au nyingine mimi kuja na hili 'bounce' ni ushawishi kutoka kwa Darassa hivyo nimeipeleka sehemu nyingine, kuna watu walikuwa wanang'ang'ania sana oohh Darassa, Darassa tunataka kitu fulani kama Darassa kwa kuwa mimi huwa siwezi ku copy nikakwepa hilo na mzigo nitatengeneza ndiyo huo. Napenda style ya Darassa kwa kuwa ni simple unamsikia neno kwa neno na kuwa na simple siku zote inauza" 

0 comments:

Post a Comment