Msanii kutoka kundi la Weusi Nikson Simon 'Nikki wa II' ameishauri mamlaka zinazohusika kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo kilicho sababisha ajali ya wanafunzi pamoja na walimu katika korongo la Rhotia Marera, Karatu siku ya jumamosi
Nikki ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa ajali hiyo Mkoani arusha iliyopelekea jumla ya watu 36 kufariki wakiwemo walimu, wanafunzi na dereva wa shule ya Lucky Vicent Academy
kupitia ukurasa wake wa Instagram Nikki ameandika kwamba,
"Lakini baada ya mazishi lazima uchunguzi ufanyike, kujuwa hali ya gari lenyewe ilikuwaje, maadili ya dereva, na hali ya usimamizi/ukaguzi wenyewe ulikuwaje..... na hii ichukuliwe kuweka udhibiti kwa watu wote walio chukuwa dhamana ya kulea watoto kwa maana ya shule...uthibiti, usimamizi..... haswa katika mazingira haya ya biashara"- Nikki wa II.
0 comments:
Post a Comment