Wednesday, May 10, 2017

Tembo wanne leo wametinga Chuo Kikuu cha UDOM Mkoani Dodoma na kuleta tafrani kubwa kwa wanafunzi wafanyakazi na wakazi wa maeneo hayo, Inaaminika ni mapito yao au shoroba na tembo husifika kwa kutunza kumbukumbu kama njia aliipita miaka 50 iliyopita anaweza kurudia palepale na inawezekana ndilo lililotokea leo hii. Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori wanaendelea kuwadhibiti ili wasilete madhara kwa wananchi.

0 comments:

Post a Comment