Wa kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa salamu za rambirambi.
Lema kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.
Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.
Mwenyekiti wa Bunge Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye.
Katika page yake ya instagram RC Gambo amewashukuru wanaarusha kwa kujitokeza kwa wingi kuwaaga watoto wetu na pia amekanusha uzushi unaoenezwa na Lema
0 comments:
Post a Comment