Monday, May 22, 2017

Image may contain: 1 person

SUMAYE NA NDOTO ZA MCHANA MPUUZENI KAFUKUZWA CRDB

Na Thadei Ole Mushi.


Sikia akili za nyumbu kila mmoja anadai kuwa kastaafu ukurugenzi wa Bodi ya CRDB ili aweze kufanya siasa vizuri. Hahahaha Sumaye anataka kufanya siasa zipi ambazo hakuwahi kuzifanya hapo kabla??

Sumaye mwaka Jana alilazwa muhimbili kwa pressure ya wananchi kuvamia mashamba yake na alipotoka alienda kwa mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ally Salum Hapi ili amnusuru mali zake hizo zisiporwe. Sumaye huyu huyu mwenye uroho wa madaraka anapata wapi ujasiri wa kuyaachia mamilioni ya crdb anayolipwa kisa kuwa mwenyekiti wa kanda ya pawani chadema ambayo halipwi chochote?? Hahahaha
#FACT

Sumaye ana ndoto kuwa Siku moja kwa sababu zake anazozijua yeye Lowassa hataweza kugombea uraisi Hivyo nafasi hiyo atapewa yeye ndicho kinachomsubirisha hapo chadema.
Kama hili ndio chaguo la pili la Chadema la kugombea Uraisi 2020 basi tayari wameshashindwa tena uchaguzi huo kabla hata mwaka miwili toka tufanye uchaguzi mkuu ukiwa haujafika.

#KWA NINI SUMAYE HAFAI KUWA RAISI?
Udhaifu mkubwa alionao Sumaye kuwa yeye ni Muasisi wa Rushwa kubwa nchini iliyopachikwa jina la TAKRIMA akiwa ccm.
Sumaye huyu huyu katika mawaziri wakuu mizigo waliokwisha kupita nchi hii huyu ni zaidi ya gunia la Misumari. Hebu chukua dk Tano fikiria ni jambo gani ambalo Sumaye alilifanya akiwa madarakani kwa miaka 10 kama utapata hata jambo moja.

Huyu ni tofauti na mawaziri wakuu wengine waliopita wote wamaacha legacy ya utumishi yeye kaacha ujinga unaoitwa Takrima. Sumaye alichofanikiwa kukifanya kwa miaka yote kumi ni kutupora watanzania Ardhi....

Sumaye huyu huyu ndiye waziri mkuu aliyekuwa na tuhuma nyingi zaidi kuliko mawaziri wakuu wengine wote. Tuhuma za kuuza bank ya NBC. Sumaye alisimamia uuzwaji wa bank hii ikiwa na thamani ya Bilion 151 yeye akaiuza bilioni 16 nani ampe uraisi??

Tuhuma za Epa, Meremeta, Kashfa ya ununuzi wa ndege ya Raisi, rada, majengo pacha ya BOT, mgodi wa Kiwira,nk zote hizi Sumaye alishiriki kamasimamizi mkuu wa serikali.
Achana na Elimu yake yenye kutia mashaka huyu hawezi kuja kuiongoza Tanzania. Yaani huyu kachafuka kuliko Lowassa.
Hayo madai yake ya kuiondoa Ccm madarkani 2020 mnapaswa kumuuliza ni nani huyo atakayesimama kuiondoa?? kama ni yeye mwambieni akojoe alale.
 
Ole Mushi

0 comments:

Post a Comment