Wednesday, June 7, 2017


Kamati kuu ya uongozi imekaa Imezingatia haya

Hatuna kipangamizi Rais kumteua yeyote

ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha kutumikia wananchi

Rais kavunja mwiko kwa kuanza kuteua wapinzani

Huu ni uthibitisho kwamba ACT ina viongozi bora hivyo inaweza kuongoza nchi.

Bado tunao wazalendo wa kutosha, hivyo raia asisite kuchagua wengine 
CCM wajifunze kupitia kwetu kuchagua viongozi bora

=>Kamati ya uongozi inamshauri Rais kuweka mfumo bora wa kuazima watu kutoka vyama vingine kwa kuweka mashauliano ili kuepuka migongano ndani ya vyama.Japo anao uwezo, hii ni kuimarisha umoja wa kitaifa

Kuteua bila mashauriano kunaleta wasiwasi miongoni mwao

ACT inampongeza Anna Mghwira kwa kuteuliwa

ACT imeona kutakuwa na mgongano kati ya nafasi yake na chama

Katiba ya ACT Wazalendo, Mama Anna Mgwhira amekoma kuwa mwenyekiti.

 Kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa hawezi fanya kazi kwa ufanisi kwa ACT- wazalendo.

ACT inamshukuru kwa kufanya kazi kwa uzalendo na ACT Wazalendo imemteua ndugu Yeremia Maganja kuwa Makamu Mwenyekiti mpya

Maswali

1. Je, hamjashauriana katika uteuzi huu?

Kama tulivyoeleza mwanzo, Rais alimteua mama wakati yupo nje ya nchi na sisi tulipata taarifa na tukamtafuta kwa mashauriano. Tumetoa tamko baada ya kushauriana na Mama Mghwira

2. Mama bado ni Mwanachama halali wa ACT Wazalendo, Kupewa ilani ya CCM mnaichukuliaje?

Rais na vitengo vyake vyote vimejilidhisha kwamba ACT ina viongozi waadilifu, huu ni ujumbe kwa watanzania kwamba ACT-Wazalendo ipo tayari kupewa nchi. Na watanzania wenyewe wameona 

Ni mujimu haya mambo yakaeleweka, tunapofanya uchaguzi, wananchi wanasoma na kuchagua ilani ambayo wanaona inafaa. Kwa hivi sasa chama kinachoongoza ni CCM na ilani inayotekelezwa ni ya CCM. Mwaka 2015 Mama Anna pia alimpa ilani ya ACT Wazalendo na tunaamini kuna mambo mazuri ya Ilani ya ACT

ACT tungeshinda tungeunda serikali ya umoja wa kitaifa, hivyo hiki kinachofanywa ni moja ya Malengo tuliyokuwa nayo.ACT tungechagua watu kutoka vyama vyote

0 comments:

Post a Comment