Posted by Williammalecela.com on Thursday, June 15, 2017
 |
Benki
kuu ya Tanzania (BOT) imepiga marufuku mchezo wa upatu ujulikanao kama
D9. Taarifa iliyotolewa na BOT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Masoko ya
mitaji na dhamana (CMSA) inasema mchezo huo ni haramu na ni kinyume na
sheria ya makosa ya jinai sura ya 16.
Hii ni kusema kuanzia sasa kile
kilichoitwa D9 kimekufa rasmi. Mtu yeyote atakayeonekana kujihusisha na
mchezo huo atachululiwa hatua za kisheria.
Nimekumbuka nilivyoshawishiwa kujiunga kwenye mchezo huo kwa kigezo cha kupata
hela "chapchap". Sikushawishika kabisa maana najua principle ya kupata
hela ni lazima uitolee jasho. Katika ulimwengu huu wa "kibepari" hakuna
pesa inayopatikana bila kufanya kazi.
Bahati mbaya kuna watu waliajiingiza kwenye mchezo huu kwa kushawishiwa
na watu wanaowaamini. Wengine wakajisajili wao na familia zao. Mtu
kajisajili yeye, mke na watoto. Kila mmoja kalipa dola 2000+, akitegemea
kuvuna dola 170 kila wiki. Leo mchezo huo unapigwa marufuku halafu
alikua hajavuna hata mara moja. What a mess.!
Ni vizuri tukawa
makini na hizi biashara za mtandaoni. Usije kuinvest pesa yako bila
kupata taarifa sahihi juu ya biashara husika. Mnakumbuka DECI?? Nayo
ilikua hivihivi. Poleni wote mliopoteza fedha zenu kupitia D9.!
|
0 comments:
Post a Comment