Polisi wakiimarisha ulinzinje ya lango la Makao Makuu ya Polisi wakati Lowassa alipokuwa akihojiwa.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amefunguka kuhusu alivyohojiwa kwa saa nne
katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
ambapo baada ya kuhojiwa ameachiwa kwa dhamana na kuondoka makao makuu
ya polisi majira ya saa 8.
Akizungumza
nyumbani kwake, Oyster Bay jijini Dar mara baada ya kutoka Makao Makuu
ya Polisi, Lowassa amesema aliitwa kuhusu kauli aliyoitoa ya viongozi wa
dini ya Kiislam wa Zanzibar (Uamsho) kuendelea kusota rumande kwa miaka
kadhaa sasa kauli ambayo inadaiwa kuwa kuwa ni ya uchochezi.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Mashinji, Edward Lowassa na mkewe Regina Lowassa.
Lowassa
aliitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa futari iliyoandaliwa na
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ambapo alisema aliwaahidi
wananchi endapo angechaguliwa kuwa rais angewatoa mashehe hao siku hiyo
hiyo lakini anashangaa viongozi hao wa dini wanavyoendelea kusota
rumande mpaka sasa bila kufahamu kosa lao.
Lowassa akifunguka, wa kwanza kushoto ni Mwanasheria wa Chadema Peter kibatala
Akizungumzia
suala hilo, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala amesema Lowassa
amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi saa 6.00
mchana.
Kibatala
amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya
onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge
huyo.
Wanahabari wakifuatikia tukio hilo.
“Mzee
amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23,
mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa
ameandika maelezo ya onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.






0 comments:
Post a Comment