Tuesday, June 27, 2017

Jumamosi ya June 24 2017 serikali ya mtaa wa Ubungo ikiongozwa na Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, ilitangaza kuubadilisha jina mtaa wa NHC Viwandani na kuupa jina la Victor Wanyama ambaye ni nahodha wa Kenya na staa wa Totteham Hotspurs.Manispaa ya Ubungo kupitia kwa serikali
ya mtaa na meya wa Ubungo waliamua kumpa heshima hiyo Victor Wanyama baada ya kukubali na kuitika wito wa kwenda kuhudhuria mechi ya mtaani maarufu kama Ndondo Cup iliyokuwa inachezwa katika uwanja wa Kinesi uliyopo Manispaa ya Ubungo.
Siku moja baadae kibao kikaondolewa kwa madai ya kuwa waliyompatia heshima hiyo Victor Wanyama hawakufuata utaratibu,  imefanikiwa kumpata katika exclusive interview meya wa Ubungo Boniface Jacob atoe majibu? ni kweli taratibu hazikufuatwa? kwa nini kibao kimeondolewa?

0 comments:

Post a Comment