MUZIKI
unachukua sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku, umekuwa ukitupa
faraja pale tunapoonekana kukata tamaa, ukitajiririsha ile furaha
tuliyonayo katika nafsi zetu na kuturejeshea kumbukumbu za kitambo.
Basi
muziki ni nini?. Muziki ni mpangilio ala na uimbaji unaoleta athari
fulani kwa kiumbe, twende pole pole hapa, yaani naweza kusema kama
msanii hawezi kupangilia ala na kuimba kwa ufundi hapo hakuna muziki.
Tusimame hapo. Kwa hapa nchi muziki wa Bongo Fleva ndio umetawala sana ukilinganisha na aina nyingine za muziki. Bongo Fleva inasikika kila kona kuanzia majumbani, mtaani, mtandaoni, kwenye vyombo vya usafiri na vyombo vya habari.
Tusimame hapo. Kwa hapa nchi muziki wa Bongo Fleva ndio umetawala sana ukilinganisha na aina nyingine za muziki. Bongo Fleva inasikika kila kona kuanzia majumbani, mtaani, mtandaoni, kwenye vyombo vya usafiri na vyombo vya habari.
Ukitaja
majina matatu ya wasanii wanaofanya vizuri katika Bongo Fleva huwezi
kuacha kumtaja Diamond Platnumz, kwa kipindi cha miaka saba aliyodumu
katika muziki huu amekuwa na mchango mkubwa sana. Kwa miaka hiyo amekuwa
akidondosha burudani ya uhakika, hakuwahi kusimama sehemu yoyote ile,
ni yeye na kazi, kazi yeye, yaani bampa to bampa kama anavyoeleza
Darassa katika wimbo wake wa muziki.
Sote
tumekuwa mashuhuda wa mafanikio yake toka alipoanza, tumeshudia akibeba
tuzo mbali mbali kama KTMA, AFRIMMA, MTV EMA na nyinginezo.
Kwanini leo Diamond?
Leo
nimevutiwa kuandika makala haya mara baada ya msanii huyu kuanzisha
wavuti ya kuuza nyimbo za wasanii ijulikanayo kama Wasafi.com. Hii ni
hatua kubwa katika muziki wa Bongo Fleva.
Nadhubutu
kusema ni hatua kubwa kwa sababu hakuna msanii mwingine aliyewahi
kufanya hivyo, yeye ameiona hiyo fursa na kuamua kuifanyia kazi. Pongezi
za kutosha kwake.Mtandao
huu unakuja kuleta ushindani mkubwa kwa mitandao kama Mdundo, Mkito na
Muziki ambayo ilitangulia kufanya biashara hiyo. Wasanii ni wengi hadi
sasa waliyokubali kuweka kazi zao katika mtandao huo. Nimemuona Prof
Jay, Navy Kenzo, Barnaba, Kasimu Mganga, Harmonize, Billnas, Saida
Karoli, Ray C, Belle 9, Chenge na Temba, Ben Pol na wengineo.Ni
wazi Diamond anazidi kujitunua kisanaa na kibiashara pia, kwa mantiki
hiyo hakuna ubishi kuwa ataendelea kuwepo katika muziki huu kwa kipindi
kirefu kutoka anafanya kazi na kundi kubwa la watu ambalo linahudumu
katika ‘sekta’ ya muziki. Kwa hiyo usitengemee jamaa atashuka kimuziki
miaka ya hivi karibuni, hilo sahau kwa sasa na ni vema ukaendelea na
mambo mengine kuliko kukaa na kuwaza hilo. Narudia teno hilo sahau kwa
sasa.Mambo
anayofanya ndiyo yanamfanya kuendelea kusalia juu. ‘Hakuna uchawi wala
ndumba’ alijisemea Prof Jay katika wimbo wake wa Zali la Mentali.
Kiufupi Diamond mwenye ametaka iwe hivyo.
Unawekeza
kutoka moyoni Aliyekuwa mtangazaji wa redio na mwandishi wa vitabu
nchini Marekani (1938-1946) Earl Nightingale aliinua mkono wake na
kuandika maneo yasemayo “watu wenye malengo hufanikiwa kwa sababu
wanajua kule wanakoelekea kimaisha.”
Wakati
Diamond anaondoka Sharobaro Records kwa Bob Junior, sehemu iliyomtoa
kimuziki alienda kuanzisha kitu kinaitwa ‘Wasafi’. Neno Wasafi lilikuwa
likisikika kwenye nyimbo zake nyingi lakini wengi walizani zilikuwa
mbwembe tu. Nani kakudanganya, tena nikupe pole sana. Diamond alikuwa
akiishi katika maneno ya Earl Nightingale, alikuwa anajua anapoelekea na
Wasafi hakuitaja tu bure, alijiona hapa alipo sasa.
Hakuna
aliyetengemea kuwaWasafi itakuja kuwa lebo kubwa nchi ya kusamimia
wasanii na kufanya biashara mbali mbali za muziki lakini ndilo tunaishi
nalo kwa sasa. Kwani ameenda kwa mganga?, wee!, tena ishia hapo hapo.
Siri ni moja tu, Diamond ni msanii aliyewekeza sana katika muziki wake,
tunapozungumzia uwekezaji si fedha pekee bali hata muda.
Kuna
baadhi ya wasanii wana uwezo mkubwa sana lakini wamekuwa wagumu
kuwekeza, mikono yao imekuwa migumu kuzama mfukoni na muda wao mwengi
umekuwa ukichukulia baadhi ya mambo yasiyokuwa na uhusiano wa moja kwa
moja na muziki wao. Moja ya nukuu kutoka kwa Anna Kleimer ni ile
inayosema, “fanya unachopenda, na penda unachofanya”. Hii kanuni rahisi
sana ambayo inawezesha watu kufikia malengo yao. Kwa asilimia kubwa watu
mwenye mafanikio makubwa dunia ni wale wanafanya yale wanayoyapenda
kutoka ndani.
Diamond
anapenda muziki wake ndio maana anamwaga fedha kuwekeza, kuna wasanii
wanafanya uwekezaji mkubwa nje ya muziki wao na wamefanikiwa huko, si
jambo baya lakini kufanya hivyo ni kumuhakikishia Diamond kuzidi
kutawala Bongo Fleva kwa kipindi kirefu zaidi, wala hakuna uchawi.
Chukua hii kwanza
Kuna
mambo huwa nikikumbuka naishia kucheka tu. Miaka kadhaa nyuma kulikuwa
kunaripotiwa visa vya mganga fulani aliyekuwa akidai ni mganga wake ni
Diamond. Mganga alikuwa akidai kuwa yeye ndiye aliyemtoa Diamond na
mafanikio yake anahusika hata ushindi wa tuzo saba za KTMA mwaka 2015
anahusika. Sikumshangaa kwa sababu hii imeshakuwa ni tabia kwa baadhi
yetu kuamini mtu anapofikia mafanikio fulani katika umri mdogo lazima
kuna jambo nyuma ya pazia.
Kiufupi
hatuamini katika juhudi binafsi. Sikuwahi kuamini katika maneno ya
mganga yule, ila nilijua hata Diamond akitetea vipi hatu hawawezi
kumuamini, lakini niliamini kuwa muda na juhudi zake ipo siku zitatupa
jibu. Muda hutoa majibu ya baadhi ya maswali yanayoshindikani katika
nyakati fulani. James Richardson raia wa Marekani alifungwa jela kwa
kusingiziwa lakini baada ya kutumikia kifungo chake kwa miaka 21
ilibainika hakuwa na hatia hivyo akaachiwa huru.
Hivi
ndivyo muda hutoa majibu yake. Sasa tunamuona Diamond katika ‘level’ za
mbali zaidi kuliko kile kipindi cha hayo maneno, je yule mganga yupo
wapi?, akiibuka tena leo wangapi watakaomuamini. Bila shaka jibu
litakuwa ‘Acha maneno weka muziki.’ Ndiyo, hilo ndilo jibu pekee kwa
sasa, kwani Diamond tunamuona jinsi anawekeza, anatengeneza ‘connection’
na watu mbali mbali wa ndani na nje na vile anavyobrand muziki wake.
Tusimame hapo kwanza.
Biashara ni wateja
Biashara
yoyote dunia inatengemea wateja ili iweze kujiendesha na kumletea faida
yule anayeimiliki au kuisimamia. Biashara ya kuuza muziki kupitia
mdandao wa Wasafi.com naiona ikimuugiza Diamond fedha nyingi kwa kuuza
tu nyimbo zake binafsi kutokana na ‘fun base’ (followers) kubwa
aliyonayo katika mitandao ya kijamii.
Diamond
ndio msanii anayeongoza kufuatiliwa na watu wengi mtandaoni kwa hapa
Bongo, watu zaidi ya milioni tano wanamfuatilia. Katika mtandao wa
instagram ana watu milioni 3.4, twitter 363,000 na Facebook milioni 2.9
(takribani milioni tatu).
Idadi
hii ya watu ndio inampa Diamond ‘kiburi’ cha kusema kwa sasa hatengemei
radio na TV kama njia ya kutangaza muziki wake. Watu milioni tano ni
wengi sana na kila siku wanaongezeka, uzuri ni kwamba jamaa mwenye kaona
fursa ndani yao. Kama nusu ya watu hao, yaani milioni 2.5 wataamua
kununua wimbo wake mmoja kupitia Wasafi.com kwa sh. 300, Diamond atakuwa
ameingiza sh, 750,000,000 (milioni mia 750). Nimegawa idadi hiyo ya
watu nusu kwa kuwa wapo wanamfuatilia katika mitandao yote mitatu.
Kwa
hesabu vilivyo wazi kiasi hiki bado mtasema ameloga au anafanya
biashara fulani ya magendo, bila shaka huu utakuwa ujinga wa kiwango cha
PhD, si bure. Hapo bado hatujaangalia ‘show’ zake anazofanya kuanzia
Bongo hadi nje, kampuni mbali mbali anazofanya nazo biashara ya
matangazo na kadhalika, kiufupi jamaa ‘kajiloga’ mwenyewe tu na hii iwe
fundisho kwa wasanii wengine.

0 comments:
Post a Comment