Thursday, June 1, 2017

 Image result for magufuli images
 Rais Magufuli: Leo nina furaha kubwa kwasababu ninapenda kukusanyiwa kodi. Inawezakana isiwe furaha kwa wakwepa kodi.


=>Baada ya kutembelea kituo hiki kwa hakika nimeridhika, nawapongeza wote waliobuni na kutengeneza kituo hiki

=>Taasisi za serikali na makampuni binafsi watakaotunza taarifa zao katika kituo hiki watakuwa na usalama.
Kituo hiki kitakuza teknolojia katika nchi yetu pia kitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.

Kituo hiki kimeanza kufanya kazi toka Oktoba lakini mpaka sasa ni taasisi tatu zimejiunga.
=>Pamekuwepo na baadhi ya wadau kufanya udanganyifu. Fedha ya serikali inatakiwa ikae mikoni mwa serikali.
Kumekuwepo na watu wanaolalamika kuonewa kubambikiziwa kodi na wanaokwepa kodi

=>Nimefurahi wakuu wa makampuni na mabenki mpo hapa maana ninyi ni walipaji kodi.
Mwaka 1992 TTCL ilikuwa haipati faida sana lakini ilikuwa inaweza kutoa divident serikalini kwa mwaka huo waliweza kulipa divident ya milioni 1.

=>Baada ya kubinafsisha na kuuza share ya asilimia 40 hatukupata divident hata siku moja. Baada ya kuona hatupati chochote tumeamua kuchukua na kununua hisa zote.

=>Ethiopia wana kampuni moja tuu ya telecommunication. Na kwa mwaka jana wametengeneza faida ya zaidi ya bilioni moja point tano dola za kimarekani.

=>Fedha walizokusanya Ethiopia ndizo walizotumia kujenga reli. Biashara yoyote lazima iwanufaishe wahusika wa nchi.
Tulitoa muongozo kwa makampuni ya simu wawe registered kwenye soko la hisa la Dar es Salaam na wamesuasua mpaka sasa.

=>TCRA wanatoa faini ndogo na inawafanya makapuni ya simu yaendelee na ukwepaji kodi.
Mimi nawaambia TCRA makampuni yasiyotaka kulipa kodi, Futa kabisa hiyo kampuni.

=>Ni lazima kila mmoja alipe kodi; awe anataka au hataki.
Niwaombe makampuni muingie katika hii data centre. Kama mtu unalipa kodi unaogopa nini kujiunga na mfumo huu?

=>Wale walio chini yangu wala siwaombi na naomba makamu wa Rais ukasimamie hili.

Mtu anaponunua vocha au kufanya transaction ya pesa ameshalipa kodi, Peleka hiyo VAT kwa serikali.

=>Ethiopia ina kampuni moja ya simu ila sisi Tanzania tuna kampuni zaidi ya saba za simu.

=>Nitolee mfano mdogo tuu, Tanzania tungekuwa na senta moja ya kupima na ku-lebel dhahabu tungepata mapato mengi sana.

=>Tungeanzisha hata vitambulisho vya machinga na tukaviuza kwa shilingi elfu kumi tungepata mapato mengi sana.

Kodi za nyumba watu hawalipi kwasababu hamna utaratibu mzuri

=>Hata hivyo nawapongeza sana vijana waliobuni mfumo huu, japo mmesema wanamefanya bure lakini najua wanalipwa mshahara. Jinsi mfumo huu utavyoendelea kusaidia kukusanya mapato tutawafikiria kuwaongeza mishahara.

=>Najua tuna data centre nyingi. Sasa nisione wizara au idara ikijenga data centre nyingine

=>Niwaombe makampuni, wafanyabiashara mjiunge na mfumo huu.
Naomba nimshukuru sana Rais wa Zanzibar Dr Shein, Makamu wa rais, waziri wa fedha, waziri wa mawasiliano

=>Narudia wito wangu kwa kuwaomba sana sana, ndugu zangu wenye makampuni ya simu muwe wa kwanza kujiunga na mfumo huu. Mimi mwenyewe namiliki laini ya Vodacom, Airtel, Tigo na TTCL.

Niwashukuru sana , Mungu Ibariki Tanzania

0 comments:

Post a Comment