Friday, June 9, 2017

Image may contain: 9 people, people smiling, people standing and outdoor
Kamanda Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini alipotembelea Rufiji majuzi na kukutana na Wananchi.
Usiku wa kuamkia leo, watu watatu wakazi wa kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti, mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Kibiti, Ndg.Gullamuhusein Kifu inaeleza kuwa miongoni mwa watu waliouawa ni mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo. Wengine waliouawa ni pamoja na Hamid Kidevu, Yahaya Makame na Moshi Machela.
Ikumbukwe juzi Askari mgambo mmoja alijeruhiwa kwa kupigwa risasi akiwa shambani, na mwingine aliuawa usiku wa siku hiyohiyo kwa kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana kabla ya kupigwa risasi maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Mauaji haya yote yanatolea ikiwa ni siku mbili tu tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alipofanya ziara wilayani Kibiti na kusisitiza umuhimu wa kulinda amani na kuzuia mauaji yanayoendelea.!

0 comments:

Post a Comment