Tuesday, June 6, 2017

Msanii wa muziki kutoka label ya ‘Mdee Music’, Mimi Mars amedai hataweza kushirikiana na dada yake, Vanessa Mdee katika kuandaa kazi ya pamoja kwa kipindi hiki kwa kuwa mashabiki wake bado wanashindwa kutofautisha sauti zao.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Dedee’ amesema kwa sasa yupo kwe wakati mgumu wa kujitofautisha na dada yake huyo.
“Mission yangu ni kujitahidi kubadilisha suala la kufanana na Vanessa, kwani mashabiki na watu wengine wamekuwa wakisema tunafanana uimbaji,” Mars alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV. “Nadhani kwa sababu bado ni mapema hawajazoea kwani mimi ni mgeni lakini niyahakikisha nakuwa tofauti ila ikishindikana kubadilika, nadhani watakuwa wameshazoea na hata kututofautisha wao wenyewe,”
Aliongeza, “Lakini niwe mkweli Vanessa siwezi kufanya naye kazi sahivi mpaka watu waweze kututofautisha ili isije ikaonekana yeye ndo kaimba wimbo wote peke yake, pia hatuwezi kuunda kundi moja la muziki bali tutaendelea kusaidiana na kuachia kazi  huko mbeleni,”

0 comments:

Post a Comment