Muigizaji wa filamu nchini, Riyama Ally amesema mume wake Leo Mysterio ndiye alimuhitaji yeye kuwepo katika video yake ‘Bonus’ na si vinginevyo.
Muigizaji huyo amekiambia kipindi cha E Newz cha EATV, mwanzo mumewe alipomueleza suala hilo alikata kwa kuwa wapo wasichana wengi wanaofanya kazi hiyo.
“Aliniambia nataka uwe video vixen, nikamwambia hapana mbona wapo wasichana wengi sana, tuwachukue, wapo wanaojuilikana na wasiojulikana na wapo kwa ajili ya kazi hii. Akaniambia, hapana hii video yangu ina stori na kama ina stori inakuona wewe, basi nilivyoiangalia nikaona kweli video inanihitaji,” amesema Riyama.
Riyama ameongeza si kweli kwamba anawaogopa ma-video queen kukaa karibu na mumewe kwani ni wanawake kama yeye, na kikubwa zaidi ifike mahali watu waamini kile ambacho kisema na si kile wanachofikiria.
0 comments:
Post a Comment