Friday, June 30, 2017

Msanii Dudubaya amewatolea uvivu wagambo wa miji tofauti nchini kwamba wanafukuzana na kina mama ntilie kuwanyang'anya vyakula wakati mapato ya wasanii na serikali yanapotea kwa kushindwa kusimamia kazi feki za sanaa  katika maeneo wanayoishi.

Akizungumza na eNewz Dudubaya amesema kwamba serikali inapaswa kulinda kazi za wasanii kwa kutumia nguvu zote kwani mwisho wa siku itajiingizia mapato kupitia sanaa hiyo hiyo. 
"Wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na Maafisa utamaduni waanzishe maduka maalumu katika kila mikoa kwa ajili ya kuuza kazi za wasanii ili kuepuka kuibiwa na maharamia. Kazi za maafisa utamaduni siyo kutoa vibali tuu vya kufanya show bali kusimamia na kukuza kazi za sanaa katika maeneo yao. Mgambo kazi zenu siyo kuwanyang'anya kina mama ntilie vyakula vyao kazi yenu ni kulinda kazi za wasanii mitaani mnapotoka" Dudubaya alifunguka. 
Aidha Dudubaya amemuomba  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa mbunifu kwa kuagiza watendaji waliopo chini yake kuandaa matamasha ya asili ili kutunza heshima ya ngoma za asili za Tanzania
"Kuna tamasha linafanyikaga Iringa kwetu ni la tamaduni na linafanyika wiki nzima huwa linafana sana  hivyo Mwakyembe anatakiwa kuwa mbuniufu na arudishe ule utamaduni wa zamani afanye matamasha ya kitamaduni  ili nyimbo za asili zirudi kama zamani zipate heshima ya Tanzania na lingine pia iwe kusimamia muziki usiibiwe ili wasanii watengeneze albamu kutengeneza  heshima" Dudubaya alikazia

0 comments:

Post a Comment