Sunday, June 25, 2017

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Hamorapa’ hivi karibuni amebambwa katika soko la  Kariakoo jijini Dar kwenye  duka moja maarufu la kuuza kanzu linaloitwa Kanzu Empire, akijinunulia kanzu kwa ajili  ya Sikukuu ya Idd.

Akizungumza na mtandao wa Global Publishers, Hamorapa ambaye aliongozana na  bosi wake, Irene Sabuka alisema  ameona ajipongeze kwa kujinunulia kanzu nzuri baada ya kufanikiwa kufunga mwezi mzima wa  Ramadhan bila kupumzika.
“ Yaani nimekuja dukani hapa  kujipongeza kwa kujinunulia kanzu nzuri  kwa sababu niliweza kufunga mwezi mzima hivyo nikaona natakiwa kwenda msikitini nikiwa nimependeza” alisema Hamorapa.

0 comments:

Post a Comment