BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa ameopoa pedeshee wa Kizungu, mwanadada
anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama ameibuka na
kufungukia ishu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na msanii huyo, kililitonya
Risasi Vibes kuwa, Maua hapendi kuweka uhusiano wake wazi kwa sasa
anabanjuka na Mzungu ambaye ndiye anayemuweka mjini kwa asilimia kubwa
na mara nyingi anapenda kuwa kwenye uhusiano na Wazungu kwani
anawapenda sana.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Risasi Vibes ilimtafuta Maua
aliyefunguka huku akiangua kicheko; “Haahaaa, jamani hayo ni mambo yangu
binafsi sitaki kuongelea, ishu za uhusiano wangu sipendi kuzianika
hadharani, tuzungumzie masuala ya kazi yangu ya muziki.”

0 comments:
Post a Comment