Wednesday, June 21, 2017

Msanii wa Bongo Fleva, Mwasiti amesema haamini kama kuna wasanii wanaotengenezwa kufanya vizuri katika muziki kwani kila mmoja anajitihada zake.

Kipindi cha nyuma msanii Afande Sele alikaririwa akisema kuna wasanii wanatengenezwa ili kufanya vizuri, huku akimtolea mfano Vanessa Mdee.
Mwasiti ameeleza suala hilo halipo kwani wasanii wanaonekana wakipambania muziki wao na yeye binafsi hajawahi kutengenezwa.
“Mimi sikai chumbaji prodyuza akanifuata chumbani kwangu turekodi bali namfuata, sikai chumbani Hanscana akanifuata tufanye video, ninamfuata nikiwa na bajeti ya kutosha,” Mwasiti ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.
“Watu hawajui kama watu wanaangaika, hakuna mtu anayetengenezwa, mimi binafsi sijawahi kutengenezwa. Nimefanya muziki wangu kwa miaka 11 right now na ninawezekana nikawa mfano kwa wazazi wengi kwa mabinti zao huko nje,” ameongeza.

0 comments:

Post a Comment