Saturday, June 10, 2017

Msanii wa Bongo Fleva, Q Chillah amesema amekuwa karibu na msanii Chid Benz kumshauri juu ya hali anayopitia kwa sasa na kuahidi rapper huyo kubadilika kutokana na kukubaliana na hali yake na kuwa karibu na Mwenyenzi Mungu

Mwimbaji huyo amekiambia kipindi cha E Newz cha EATV kuwa Chid Benz ambaye amekuwa akipambana kutoka kwenye wimbi la matumizi ya dawa za kulevya, yupo katika hali nzuri na hivi karibuni watu watengemee wimbo wao wawili.
“Nilichokifanya mimi nikumsongeza Rashid Karibu na Mwenyenzi Mungu kwa sababu tunaishi lakini ni lazima ujue kuna Mwenyenzi Mungu, kwa hiyo wamtarajie Rashid mwingine tofauti na yule na mpaka nilifanya nae  (wimbo) ni kwamba nimeona nuru  kwake,” amesema Q Chillah.
“Rashid ni rapper mzuri ingawa amepitia katika hali ambayo hata mimi niliwahi kupitia. Dawa ya Rashid anayo yeye mwenyewe hatuna sisi, na tiba ni kukubaliana na nafsi yake kwamba yupo kwenye kiza anahitaji kwenda kwenye nuru,” ameongeza.
Q Chillah amesema anachofanya sasa ni kujaribu kumpa Chid Benz nafasi ya pili wakati huu yupo hai na kuwataka wana hip hop na Watanzania wenyewe amani upendo wajaribu kuangalia watu waliofanya makosa na wanaojaribu kurudi tena wawape nafasi.

0 comments:

Post a Comment