Thursday, June 22, 2017

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi mashukakwa Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar esSalaam Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wa pili Kushoto ni Malkia wa Taarabu Hadija Kopa na kuliani Muigizaji maarufu wa tamthilia ya Huba Riyama Ali ambao ni mabalozi maalum wa DStv. Haflahiyo iliyofanyika mapema leo katika kituo hicho ambapo vifaa mbalimbali vyenye thamani yashilingi milioni mbili vikiwemo vyakula, mashuka, vyombo na mitungi ya kuzimia moto vilikabidhiwa


Mshonaji katika mradi wa ushonaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madinnahcha Tandale jijini Dar es Salaam Aziza Amri (wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu mradi huounaofadhiliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania. Kutoka kushoto ni Malkia wa mipasho HadijaKopa ambaye ni balozi maalum wa DStv, BiKuruthum Juma ambaye ni mkuu wa kituo hicho, Baraka Shelukindo Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania na kulia ni Muigizaji maarufu watamthilia ya Huba Riyama Ali. Mbali na kutembelea mradi huo, Multichoice pia ilikabidhi vyakula navifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa kituo hicho
Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa zawadi ya sikukuu ya Idi kwa kituo cha kulelea watotoyatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam. Msaada huo wa vyakula na vifaambalimbali umekabidhiwa kwa kituo hicho na Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo ambayo pia ilihudhuriwa na mabalozi kadhaawa DStv akiwemo malkia wa Taarab Khadija Kopa na muigizaji maarufu wa filamu na Tamhtilia yaHUBA , Riyama Alli.



Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Shelukindo amesema kwa takriban miaka mitanomfululizo Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho kwa mambo mbalimbali. Amesemawanafanya hivyo kwa kutambua kuwa malezi ya watoto waishio katika mazingira magumu nijukumu la kila mtu na kila taasisi. “Tunatambua kuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawaambao kwa sababu moja ama nyingine wamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa nindugu zetu, watoto wetu, na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo kuwasaidia ni jukumu letu”



Amesema mbali na kwamba Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho mara kwa mara kwakuwapa vyakula na mahitaji mengine, lakini pia waliamua kufadhili uanzishwaji wa mradi waushonaji ambao unakisaidia kituo hicho katika kujiingizia kipato. “Tunajua kuwa chakula, malazi namambo mengineyo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya vijana wetu, lakini pia tuliona ni busarakuwawekea kamradi japo kadogo ambako wataweza kujipatia kipato. Tumefurahi sana kuonamradi huu unaendelea na tunaamini kuwa wataweza kuuendeleza na kuukuza ili uwasaidia Zaidi.”Alisema Shelukindo.



Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho Mama Kuruthum Juma ameishukuru MultichoiceTanzania kwa msaada wao wa mara kwa mara kwa miaka mingi sasa. Amesema kitendo chaMultichoice Tanzania kukisaidia kitua hicho kwa mambo mbalimbali hususan mradi wa ushonajikumewasaidia sana katika kujipatia kipata japo kusaidia gharama za uendeshaji kituo hichoambazo ni kubwa. “Kwa kweli gharama za uendeshaji kituo ni kubwa sana na kamamnavyofahamu watoto wanaolelewa hapa hawana uwezo na wengi wao hawana wazazi, hivyo nijukumu letu kuwalea, kuwapa matibabu, na pia kuwasomesha, hili kwa kweli ni jukumu kubwa natunahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali” alisema Mama Kuruthum



Amesema idadi ya watoto imekuwa ikiongezeka lakini kituo hakina uwezo mkubwa kutokana naufinyu wa eneo na bajeti hivyo akawaomba wadau wengine kuangalia uwezekano wa kukisaidiakituo hicho ili kiweze kuhudumia watoto wengi Zaidi.



Naye Malkia wa Taarabu – Khadija Kopa amesema amefarijika sana kuona Multichoice Tanzaniainawajali watoto hususan wale waishio katika mazingira magumu ambao aghalabu husahaulika najamii. “Kwakweli Multichoice Tanzania wamefanya jambo la maana sana. Ni vyematukaunganisha nguvu zetu kuwalea hawa watoto wetu kwani nao wana haki kama watotowengine” alisema Kopa.



Naye muigizaji Riyama Ali amepongeza jitihada zinazofanywa na Multichoice Tanzania pamoja nauongozi wa kituo cha Almadinna katika kuwasaidia watoto hao. “Watoto hawa ni hazina ya taifa.Tukiwasaidia hawa wakakua vizuri, wakapata elimu nzuri, kesho na keshokutwa tutapata wabungehumu, mawaziri, wakurugenzi, wanamichezo, wasanii na kadhalika. Tushirikiane kuwalea na hili nijukumu letu sote na ni kitu kinacholeta Baraka” alisema Riyama.





Kituo cha Al-Madinnah Orphanage Centre kilianzishwa mwaka 2004 na kwa hivi sasa kituo hichokinahudumia jumla ya watoto 65 ambapo 40 kati yao ni wavulana na 25 wasichana na wengi waoni wanafunzi wa shule za msingi.

0 comments:

Post a Comment