
Mwanaume
mmoja aliyebadili jinsia ni wa kwanza barani Ulaya kujifungua mtoto
baada ya kuwa mjamzito kwa njia ya kupandikiziwa mbegu za kiume.
Alisisitiza
kujifungulia nyumbani sababu alikataa kuorodheshwa kama mama kwenye
nyaraka zozote za hospitali - hitaji la kisheria nchini Ujerumani. Baba
huyo, ambaye alibakisha viungo vya uzazi vya mwanamke, amekuwa
akifanyiwa tiba za kubadilishwa homoni kwa miaka kadhaa kubadili jinsia.
Habari
zaidi kuhusu upandikizwaji mbegu au taarifa za uhusiano wowote
zimehifadhiwa kutolewa hadharani kutokana na baba huyo kutaka kumlinda
mtoto wake huyo.
Rasmi mtoto huyo, ambaye alizaliwa Machi 18, hana mama, ana baba pekee.
Msemaji
wa Mambo na Ndani wa Berlin alisema: "Mtu huyo aliyezusha maswali
hakutaka kujitokeza kama mama ila baba kwenye cheti cha kuzaliwa na
matakwa hayo yameheshimiwa."
Baba
huyo mtarajiwa pia alitaka kwamba jinsia ya mtoto huyo 'isifichuliwe
kwa namna yoyote'. Lakini mamlaka zilipuuza hilo na kutangaza kuwa ni wa
kiume.
Vyombo vya habari vya Ujerumani viliibuka kwa namna ya kushangaza katika habari ya uzazi huo wa kubadili jinsia.
'Baby
belly instead of a beer belly!' (Kitambi mtoto badala ya kitambi bia!")
kilikuwa moja ya vichwa vingi vya habari kwenye magazeti ya Ujerumani
yakiripoti kuzaliwa kwa mtoto huyo.
Wakati
huohuo, Falko Liecke, diwani wa wilaya hiyo ambako mtoto huyo
alizaliwa, alisema: "Hiki ni kitu ambacho sikuwahi kusikia maishani ana
kushuhudia."
Mwaka
2011 Mahakama Kuu ya Ujerumani iliamuru kwamba mtu binafsi hatakiwi
kuondolewa viungo vyake vya uzazi awe mwanamke au mwanaume 'kupata
kutambuliwa hadharani kisheria kwa jinsia atakayowekewa'.
Ndio maana baba huyo wa mtoto wa hivi karibuni amekuwa mwanaume wakati akiendelea kuwa na viungo vyake vya uzazi vya kike.
Dk
Tobias Pottek wa Hospitali ya Asklepios West mjini Hamburg alisema:
"Hata kama mwanamke anataka kuishi kama mwanaume na kuwekewa homoni
kuotesha ndevu, kwa kuwa mji wa mimba na mayai bado yapo, pia
inawezekana kupata ujauzito.
Hili
ni jambo la kwanza la mtoto kuzaliwa barani Ulaya wa mzazi aliyebadili
jinsia, lakini katika Marekani jambo la Thomas Beatie, mwanaume
aliyebadili jinsia ambaye alikuwa na watoto watatu, linafahamika mno.
Beatie
alikuwa akidai talaka kutoka kwa mkewe, lakini alikataliwa sababu jaji
hakuweza kuthibitisha kama alikuwa mwanaume wakati akifunga ndoa.
Jaji huyo aliamua hakukuwa na mamlaka ya kisheria ya kuomba talaka kama ndoa hiyo haikuwa ikitambuliwa.
0 comments:
Post a Comment