Mkazi
wa kijiji cha Kate, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, amejikata uume wake
kwa kisu kwa hasira baada ya kuota kuwa anafanya mapenzi na mke wake
aliyefariki mwaka mmoja uliopita.
Mwanaume
huyo mwenye umri wa miaka 58 alijikata uume wake juzi majira ya saa
4:00 asubuhi akiwa amejifungia chumbani kwake peke yake.Mwenyekiti wa
Kitongoji hicho Richard Mselema, akizungumzia tukio hilo alisema kuwa,
mtu huyo alikuwa akitafuta binti wa kumuoa na kuishi nae kwa muda mrefu
baada ya mke wake kufariki, lakini wanawake wamekuwa wakimkataa kwa kuwa
umri wake ni mkubwa.Baada ya kufanya tukio hilo akiwa peke yake na
kupata maumivu makali, mwanaume huyo alipiga yowe na watu walipofika na
kumkuta anavuja damu nyingi sehemu ya uume wake huku kisu kikiwa
kimetupwa pembeni, waliamua kumbeba na kumkimbiza katika Zahanati ya
Kate Mission.Kwa mujibu wa daktari wa zamu, Paul Katindi, aliyempatia
matibabu katika majeraha aliyoyapata, alisema kuwa hali yake itakuwa
nzuri na anaweza kuendelea na mchakato wake wa kumtafuta mwanamke wa
kuoa.“Niliamua kujikata kutokana na kuwa na uume lakini siutumii kwa
kuwa sina mke wala mpenzi. Hivyo sikuona umuhimu wala faida ya kuwa
nao.” Alisema majeruhi huyo alipoizungumza na mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya ya Nkasi, Zeno Mwanakulya, ambae pia ni jirani yake,
alipokwenda kumtembelea na kumpa pole.
0 comments:
Post a Comment