Mzee
mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 83 amekutwa amekufa pembezoni ya
kaburi la mke wake baada ya kujipiga risasi ya kichwa katika makaburi ya
St. John yaliyopo katika kijiji cha Middle jijini New York,
Marekani.Mzee huyo ambaye alitambulika kwa jina la Robert Gallo alikuwa
amekwenda eneo hilo
kwa ajili ya kutembelea kaburi la mke wake lakini baada ya muda mlio wa risasi ulisikika na walinzi wa eneo hilo walipokwenda kuangalia nini kimetokea walimkuta akiwa amelala chini pembeni na kaburi la mke wake.

Msemaji
wa makaburi ya St. John alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa mzee
Gallo kupoteza maisha kwani walikuwa wamemzoea kumwona mara kwa mara
kutokana na utaratibu ambao alikuwa amejiwekea wa kwenda katika kaburi
la mke wake.
“Wafanyakazi
wengi wa makaburi haya wanamjua vizuri, huwa anatembelea kaburi la mke
wake mara kwa mara,” alisema msemaji wa makaburi hayo na kuongeza
“Tumesikitishwa na jambo ambalo limetokea na tunamwombea yeye pamoja na
familia yake.”
0 comments:
Post a Comment