NAMBA
za magari ya msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’,
zinahusishwa na baadhi ya mashabiki wake kuwa ni za Freemason kutokana
na kuwa za aina moja inayosomeka 966.
Uvumi
juu ya kumhusisha Nay na taasisi hiyo inayosadikika kumuabudu Shetani
zilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha za magari yake
kusambaa mtandaoni, lakini alipotafutwa na safu hii ya burudani
kuzungumzia tetesi hizo Nay alisema kuwa;
“Watu
wanaongea vitu ambavyo hawavifahamu, mimi na Freemason wapi na wapi,
hiyo namba ni namba ambayo huwa napenda kuitumia tu na kwa watu ambao
wanasikiliza nyimbo zangu watakubaliana nami kuwa huwa napenda kuitaja,
kiukweli haina uhusiano wowote na Freemason,” alisema Nay wa Mitego.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment