Tuesday, June 27, 2017

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ahojiwa kwa tuhuma za Uchochezi. Aachiwa baada ya kujidhamini, atakiwa kuripoti tena Alhamis.
Lowassa anadaiwa kutoa kauli za kichochezi mbele ya waumini waliohudhuria futari. Aidha mahojiano baina ya Ofisi ya DCI na Mwanasiasa huyo yamedumu kwa saa nne.Mjumbe wa kamati kuu na mgombea urais mwaka 2015 ndugu Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya Polisi saa nne kama alivyoambiwa na DCI.Lowassa alikuwa amefuatana na Magari manne ya kwake pamoja na magari mawili ya polisi wenye Siraha.
Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji. Aliwasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.
Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.
Kwa lolote litakalotokea tutazidi kujuzana.
Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.

0 comments:

Post a Comment