Rapa Nikki wa Pili kutoka 255, amewataka wasomi kuacha kuilalamikia serikali kwa kukosa ajira badala yake watumie elimu waliyopata katika kujiajiri.
Nikki amesema hayo kupitia kipindi cha Supamix cha EA Radio kuwa wanafunzi wengi wanaonyesha kukata tamaa ya maisha kwa kile kinachodaiwa ukosefu wa ajira.
“Kwa sasa kuna uhakika wa kupata elimu katika nchi yetu, kufa masikini kwa sababu hakuna uthubutu kwa waliohitimu masomo yao, wamekuwa wakisifia sana akili kuliko uthubutu. Wanaobadilisha dunia ya leo ni wale wenye kuthubutu kuhusu jambo fulani” amesema Nikki moja ya memba wa kundi la muziki la Weusi.
Nikki pia ameongezea kuwa “Watu wenye diploma na degree ndiyo wanaongoza kwa kulalamika hakuna ajira huku waliomaliza darasa la saba wanapambana katika kutafuta pesa”.
Hata hivyo rapa huyo amewashuri vijana waliopo vyuoni wahakikishe wanapata elimu ya vitu kutoka nje ili wakirudi mtaani isiwe kazi kwao.
0 comments:
Post a Comment