NDANI ya
tasnia ya burudani Bongo, kwa sasa imevamiwa na wingi wa wasanii, wauza
sura na wanamitindo wapya ambao wamejipatia umaarufu ndani ya muda
mfupi hasa kutokana na kukua kwa kasi kwa mitandao ya kijamii.
Wakiitumia mitandao hiyo kujitangaza, wamekuwa hawalali kwani ‘njaa’ yao
kubwa ni mkwanja, tofauti na wadada wa kipindi cha nyuma ambao walitaka
sana umaarufu, huku pesa ikiwa ni chaguo namba mbili. Wafuatao ni
baadhi ya wanadada ‘hot’ wanaokutana kupitia kazi mbalimbali za sanaa ambao pesa zinawatoa akili na wako tayari kufanya lolote lile ili kupiga mkwanja.

LULU DIVA
GIGY MONEY
Huyu ni muuza sura kwenye video za Kibongo, ameonekana kwenye video
nyingi zikiwemo, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego na Inde ya Dully
Sykes. Tofauti na kuuza sura, msichana huyu ni msanii akiimba wimbo
uitwao Supu aliomshirikisha Matonya. Pia mtangazaji. Kuhusu kusaka pesa,
Giggy anasema kuwa yuko tayari kufanya lolote lile kwa sababu dunia ya
sasa kila kitu ni pesa na kama mtu hana mkwanja na thamani hana. “Maisha
yamepanda na kila kitu ni gharama. Aisee kwenye pesa, bora punda afe
mzigo ufike, niko tayari kupiga dili yoyote ile ya halali ndiyo maana
natumia kila kipaji alichonijalia Mungu ili kuhakikisha nakamata
mkwanja,” alisema Giggy.

LULU
DIVA Ukitaja mavideo ‘vixen’ wakali kwa sasa Bongo, jina la mwanadada
huyu haliwezi kukosekana. Ndiye ‘Official video queen’ kwenye kichupa
cha wimbo uitwao Naogopa wa Mirror aliomshirikisha Barakah The Prince.
Mwanadada huyu pia ni muigizaji na ameonekana kwenye muvi iitwayo Nikabu
ya Kitale. Katika kutengeneza mkwanja, mara kadhaa amenukuliwa akisema
hawezi kuweka usistaa du, anasaka mkwanja kwa kila hali na haachi
kujichanganya, maana akiwa hana mkwanja hujihisi nusu chizi! HAITHAM
Huyu ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao kazi zao zimebahatika kupata
‘air time’ nzuri kwenye media
yingi.
“Unajua kwenye maisha ya sasa huwezi kuwa tegemezi kabisa. Mara
mapedeshee au wazazi. Inafikia hatua kila kitu unatakiwa kufanya
mwenyewe. Kwa upande wangu pesa ni kila kitu na sanaa sifanyi kwa
kumfurahisha mtu,” anasema.
ERYCAH
Si jina geni kwa wapenzi wengi wa burudani Bongo. Tofauti na kuonekana
kwenye kichupa cha Wimbo wa Saka Hela wa Mbongo Fleva, Linex, mwanadada
huyu amewahi kukwaa skendo ya kutoka kimapenzi na mshikaji huyo, kabla
ya kukanusha. Erycah ana diploma ya Record Management aliyoipata chuoni
Magogoni, anasema mbali ya elimu, ameamua kujiingiza katika kuuza sura
kwenye video kama biashara zingine na malengo makubwa ni kudaka mkwanja.
“Dunia ya sasa imebadilika, wanadada hatutakiwi kuchagua kazi.
Kama sina pesa kiukweli wakati mwingine huwa nahisi hata kuumwa,” anasema Erycah.
AMBER
LULU Jina la mwanadada huyu machachari ni maarufu sana kwenye mitandao
ya kijamii hasa Instagram. Kabla ya kufahamika anajihusisha na ishu gani
hapa mjini, umaarufu wake ulitokana na skendo za kupiga picha za nusu
utupu alizokuwa anazitupia kwenye mitandao na baadaye akaanza mishe za
uvideo queen. Kuhusu mkwanja, Amber Lulu anasema bila kuwa nao, hakuna
kinachofanyika kwenye maisha ya mwanadamu wa leo. “Mh! Pesa ndugu yangu
hata hakuna maneno ya kuizungumzia yakaisha, so kama sina pesa kwa nini
nisiwe nusu chizi!” alimaliza Amber
0 comments:
Post a Comment