Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa
Freeman Mbowe amekanusha kuhusika katika sauti ya maongezi inayosambaa
kuwa yupo katika mahusiano ya kimapenzi na Staa wa filamu ‘Wema Sepetu’.
Sauti hiyo iliyosemekana kuwa ni Wema na Mh. Mbowe ilisambaa kwa kasi
kitendo ambacho Wema Sepetu alijitokeza kwa kupost maelezo katika picha
kupitia akaunti yake ya Instagram na kukanusha kuwa sio yeye na
inonekana wazi kuwa kuna mtu aliyehusika kuigiza sauti yake kwa lengo la
kuchafua majina ya wanaohusishwa.
“mimi ninalichukulia kama taarifa za kawaida ya maji taka ambazo
zinasambazwa, taarifa ambazo zinategenezwa hazina ukweli wala hazina
msingi wowote ndo ambacho naweza kusema kwa sasa kwasababu hizo taarifa
sio za kweli…timu yangu ya mtadao inajaribu kufatilia kujua
zimeoriginate kwa nani” Amesema Mh. Mbowe katika simu na Perfect.
Hata hivyo Mbowe amesisitiza kuwa hajawahi kuwa katika mahusiano ya
kimapenzi na Wema Sepetu na kubainisha kuwa kwasasa hana chochote
anachoweza kuzungumza kwakuwa jambo hilo liko katika mikono ya
wafatiliaji ili kujua nani amehusika.

0 comments:
Post a Comment