Thursday, June 22, 2017

Video Queen na muimbaji ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amejipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Nampa Papa’ uliotayarishwa na procuder Kimambo Touches.

Utakuwa ni wimbo wa pili wa muimbaji huyo baada ya mwaka jana kuachia wimbo ‘Supu’ ambao ulifanya vizuri kwa kiasi chake.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Jumanne hii Gigy amesema wimbo huyo ni wimbo ambao unamfanya mwanamke kujivunia urembo wa pekee aliyopewa na Mungu.
“Nampa Papa ni wimbo fulani kama nyimbo zangu zilizopita, ni kama Supu nilikuwa najivunia maumbile yangu. Kwahiyo kwenye ‘Nampa Papa’ ni wimbo fulani ambao bila shaka kila mtu ataufurahia,” alisema Gigy.
Aliongeza, “Kwahiyo mabibi na mabwana tukae mkao wakula Gigy kaleta balaa jingine jipya tuoneshe ushirikiano na thamini vya nyumbani. Pia wimbo huu sijaandika mwenyewe nimeandikiwa na mwanangu mmoja anaitwa Marioo,”

0 comments:

Post a Comment