Posted by Williammalecela.com on Thursday, June 15, 2017
 |
*UVCCM WAMPA ZA USO LOWASSA.*
*Wamuambia ni Mkongwe wa kuzua mambo.*
Mwandishi wetu, Dar Es Saalam.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umemtaka Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa kuacha uongo kwani
hana historia ya kupigania maslahi ya umma.
Aidha, imesema madai
ya lowassa kwamba aliwahidi wananchi angeunda Tume ya kupitia mikataba
ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka kujitafutia umaarufu
wa kisiasa.
Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi
video ya matamshi yake wakati akiwa katika mkutano wa hadhara
akihutubia mkoani Geita ikionyeaha kama kweli alitoa matamshi hayo.
Hayo yalielezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga jijini Dar
Es Salam.
alisema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au
kuzungumzia mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma kwasababu
hata kujiuzulu kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa
na sakata la ufisadi.
Shaka alibainisha kuwa hakuna ushahidi
wala kumbukumbu inayoonyesha kuwa Lowasa siku moja aliwahi kutetea
maslahi ya umma wakati akiwa serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa
Waziri Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
"UVCCM
tumemestushwa na matamshi ya Lowasa yanayodai wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu akiwa Mkoani Geita kuwa aliwahi kutamka kama angeshinda
urais angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini , hakuna ushahidi huo
na hawezi kuthibitisha ni uongo mtupu "Alisema Shaka.
Shaka
alisema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati alipokuwa waziri mkuu
angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais iundwe Tume lakini
alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama anavyotaka
kuwaaminisha wananchi baada ya kuona Rais John Magufuli akiungwa mkono
kitaifa na kimataifa.
Kaimu huyo Katibu mkuu alikumbushia kuwa
alichosikika akisema Lowasa ni kwamba akiwa Rais atawakaribisha
wawekezaji zaidi pamoja na marafiki zake wenye nguvu za fedha na mitaji
mikubwa ili kuiendeleza migodi na uchimbaji wa madini ambayo
itamtajirisha kila wananchi bila kuelezea mbinu za utekelezaji huo.
"Waziri pekee jasiri, mzalendo na aliyekuwa mchapakazi kwa bidii
katika serikali ni Dk Magufuli kwani hata Lowassa alipomnadi Dk
Magufuli wakati akiwania ubunge mwaka 2005 alimtaja mbele ya wananchi
kwamba ni jembe na turufu muhimu "Alisema Shaka.
Aidha alieleza
sifa peke ya Lowassa akiwa serikali ni tabia yake ya kumshauri jambo
Rais na kama litafanyika, hugeuka na kuwaambia watu kwamba yeye ndiye
akiyemshauri Rais na kama si yeye kisingefanyika.
Shaka alisema
upo ushahidi kwamba aliwahi kumshauri suala fulani Rais mstafu Mzee
Ali Hassan Mwinyi kisha akawaambia wapambe wake kwamba yeye ndiye
aliyeshauri kitendo kilichomfanya Mwalium Julius K. Nyerere amwite
kilichjambo lililomfanya mwalimu Julius Nyerere amwite Lowassa nyumbani
kwake msasani na kumkanya.
"Lowasa aliitwa mbele ya aliyekuwa
Katibu Mkuu wa UVCCM Sukwa Said Sukwa nyumbani kwa mwalimu Msasani
akasemwa vikali sana na mwalimu kwa kitendo hicho pia akaonywa aache
kutumia magazeti kusaka uongozi na umaarufu"Alieleza Shaka
Pia
Shaka alimtaka Lowassa kuacha tabia ya kutaka kuvika joho lisilo na
hadhi yake na akumbuke tuhuma ambazo amewahi kurushiwa na viongozi wa
chadema wakipita huku wakimnadi nchi nzima haziwezi kufutika kwa mtindo
anaotaka wa kujifagilia kwa uzushi.
Hata hivyo kaimu katibu mkuu
huyo alisema si kweli kama ujasiri, uzalendo na utashi wa kutaka
kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kupambana na ufisadi na kupitia mikataba
michafu haiwezekani kufanyika bila katiba mpya kama anavyodai Lowasa.
"Ujasiri, uzalendo na uthubutu wa kutenda mambo yoyote magumu
hakuhitaji mabadiliko ya katiba , aidha kwa kuwepo wa katiba mbaya au
nzuri kwasababu vitu hivyo havishabihiani , katiba iliopo ni nzuri na Dk
Magufuli ataleta maajabu ya kihistoria chini ya katiba ya sasa
"Alisisitiza Shaka
Alimtaka Lowasa kufuta ndoto na matumaini
kwamba itatokea siku moja akawa Rais wa nchi hii na kuacha kueneza
uzushi kuwa alikatwa jina lake kwa kumhofia angepitia mikataba ya
madini.
"Jina la Lowassa liliondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo
matumizi mabaya ya madaraka, viongozi wa CHADEMA kumnanga nchi nzima
pamoja na ukiukaji wake wa taratibu, miiko na maadili huku akitumia
nguvu za fedha kutaka ateuliwe jambo ambalo CCM imelikataa "Alisema
Shaka .
Baadhi ya vyombo vya habari jana vilimnukuu Lowassa
akimpongeza Rais Dk Magufuli kwa kuunda Tume ya kupitia mikataba ya
madini huku akijigamba naye aliwaahidi wananchi wakati kampeni akiwa
mkoani Geita kwamba akishinda urais angeunda Tume jambo ambalo pia
lilifanya jina lake kukatwa ndani ya CCM.
Source Uhuru 15/06/2017
|
0 comments:
Post a Comment