Nchi ya Russia imeingia matatani baada ya kutakiwa kutoa maelezo kutokana na watu wawili raia wa Russia kujichora rangi nyeusi ili waonekane kama Wacameroon,watu hao walikuwa katika sherehe za kuitangaza michuano ya Mabara ambayo hufanyika kabla ya Kombe la Dunia.
Tukio hilo limetokea kati ya mmoja ya watu hao ambaye ni mwanamke alikuwa amejipamba kwa kuvaa ndizi hali inayoashiria dharau au ubaguzi kwa watu wenye asili ya Afrika.
Baada ya picha hizo kumekuwa na mijadala mingi na kwa kuwa Russia ndio waandaji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 inatakiwa kuwa makini na suala la ubaguzi huku swala hilo likiwa limezua gumzo zaidi.Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itafanyika Russia ambayo kwa mujibu wa viongozi wa soka wa FIFA wamesema tayari ilishaelezwa Russia kutoa mafunzo kwa watu wake kuhusiana na ubaguzi wa rang


0 comments:
Post a Comment