LALITA Ben Bansi, aliyeathiriwa kwa shambulio la tindikali nchini India, amejikuta katika kilele cha furaha wakati akifanyiwa harusi yake mjini Mumbai hivi karibuni."Hakuna ambaye angetarajia kwamba baada ya kuunguzwa kwa tindikali na kufanyiwa upasuaji mara 17 nitaweza kupata mpenzi. Lakini sasa mambo ni tofauti, naolewa," ameliambia gazeti laHindustan Times katika sherehe iliyofanyika huko Thane.Kilichotokea ni kwamba alipiga simu kwa lengo la kumtafuta mtu mwingine, lakini akakosea namba na kumfikia mtu mwingine.Msichana huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyeshambuliwa na jamaa yake mnamo 2012, amesema kwake kufanikiwa kupata mpenzi ni kama miujiza mkubwa kwake."Lalita alipiga simu yangu kwa bahati mbaya miezi mitatu iliyopita. Nilimpigia tena baada ya siku 15," Singh, mwenye umri wa miaka 27, anayefanya kazi na kampuni ya CCTV ameliambia gazeti la The Hindu."Tulizungumza na nikaipenda sauti yake. Tuliendelea kuzungumza kila siku na ni hapo ndipo nikamuomba kumuoa," anafafanua.
Wakati wa mazungumzo yao, Lalita alimfahamisha Singh kwamba yeye ni muathiriwa wa shambulio la tindikali."Lakini nilimuambia kwamba ninampenda na ningependa kumuoa. Wachumba wengi hupendana kwa sababu ya sura na mwishowe huishia kutalikiana. Lakini kwake sikuvutiwa na sura, yeye ni mtu mzuri, naomba Mungu atubariki maisha yetu yote," aliongeza.
Harusi yao imehudhuriwa na nyota wa filamu za Bollywood akiwamo muigizaji Vivek Oberoi, aliyekutana na Lalita katika hafla iliyoandaliwa kwa waathiriwa wa mashambulio ya tindikali.
Nyota huyo alimtaja bi harusi kuwa "shujaa wa kweli". Alimsifu bwana harusi pia kwa kumpenda namna alivyo.
Inakadiriwa kwamba nchini India, kuna mashambulio 1,000 ya watu kumwagiwa tindikali kila mwaka, licha ya kwamba inadhaniwa visa vingi haviripotiwi.
0 comments:
Post a Comment